Category: News
Wananchi Sasa Kujipima Virusi Vya Ukimwi – Waziri Ummy Na Wamjw- Katavi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amesema kuwa bunge la Tanzania limerasimisha sheria ya Wananchi kuweza kujipima wenyewe maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
Waziri Ummy amesema hayo leo Disemba 20 katika ziara ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na ujenzi wa miundombinu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, ikiwa ni jitihada za Serikali za kuboresha huduma za Afya nchini.
“Napenda kuwapa Habari njema kuwa Bunge la Mwezi wa 11 limepitisha Sheria, kwahiyo sasa ni rasmi Tanzania mtu kujipima maambukizi ya VVU mwenyewe, kwahiyo hivi vitendanishi (vifaa) vitakuwa vinauzwa kwenye maduka, pia kugawa bure baadhi ya maeneo kwa sababu wakati mwingine watu wanaona unyanyapaa kwenda kupima wenyewe,” Amesema Waziri Ummy.
Ameendelea kusema kuwa, Serikali imeweka angalizo kuwa, kujipima mwenyewe sio majibu ya mwisho, hivyo kuwataka wananchi kuwa, baada ya kujipima wanatakiwa kwenda katika vituo vya kutolea huduma za Afya kwa ajili ya kuthibitisha na ushauri zaidi wa jinsi ya kuishi.
Aidha, Waziri Ummy ameagiza kuendelea kutoa elimu ya Afya kwa wananchi, hususan watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kutumia dawa kwa usahihi kulingana na maelekezo ya Watoa huduma za Afya katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini.
“Tuendelee kuhakikisha watu wote waliobainika na ugonjwa wa Ukimwi, waendelee kutumia dawa kwa usahihi kama walivyoelekezwa na Wataalamu wetu katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini”. amesema Waziri Ummy.
Mbali na hayo, amesema kuwa kuna changamoto ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 24, huku akiweka wazi kuwa kitaifa hali ya maambukizi mapya kwa vijana hao ni asilimia 40%, huku vijana wa kike ikiwa ni asilimia 80 na wakiume ikiwa ni asilimia 20.
Kwa upande mwingine Waziri Ummy amewatia moyo wanaoishi na maambukizi ya VVU kwa kuwakumbusha kuwa, kuhudhuria katika vituo vya Afya na kufuata maelekezo kama walivyopewa na Watoa huduma, pia kuishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi sio mwisho wa maisha.
“Niendelee kuwatia moyo kuwa na maambukizi ya Ukimwi sio mwisho wa Dunia, sio sentensi ya kifo, sikuhizi watu Wanaishi vizuri, kwahiyo nawahimiza kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya, kupima na kuanza kutumia dawa”. Amesema Waziri Ummy.
Nae Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi, ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi Lilian Matinga amesema kuwa, hali ya upatikanaji wa dawa ipo vizuri Mkoani hapo, huku akidai kuwa kwa mwaka 2017/2018 bajeti ya dawa na vitendanishi ilikuwa Bilioni 2.9 na kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Mkoa umetengewa jumla ya shilingi Bilioni 3.97 ikiwa ni ongezeko la shilingi Milioni 460.07. Aliendelea kusema kuwa, kwa sasa hali ya upatikanaji wa dawa muhimu ni zaidi ya asilimia 90% katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini. alisisitiza.
Siku ya UKIMWI 1 Disemba 2019-Mkoani Mwanza, Tanzania
Hadi sasa Watanzania milioni.1.4 wanaoishi na VVU ambapo kiwango cha maambukizi kikiwa ni asilimia 4.7 ikilinganishwa na asilimia 7.0 ya mwaka 2014.Hayo yamesemwa leo na Mgeni rasmi wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya UKIMWI duniani na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemevu Mhe. Jenista Mhagama jijini hapa. Waziri Mhagama amesema kuwa maambukizi mapya na vifo vitokanavyo na UKIMWI pia yamepungua.
“Tumeweza kupata mafanikio haya kufuatia kuboreshwa kwa huduma.za ART na afua za kinga kama vile utahiri wa kitabibu wa wanaume na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto”, alisema Waziri Mhagama.Aidha, amesema kiwango cha watu wanaoishi na VVU walioko kwenye mpango wa ARV kimeongezeka kutoka asilimia 22 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 57 ya mwaka 2017.
Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema mpaka kufikia mwezi Septemba 2019 takribani watu 1,252,205 kati ya wananchi 1,600,000 wanaokadiriwa kuishi na VVU nchini walikuwa wamepima na kufahamu hali zao za maambukizi ya VVU.”Hii ni sawa na asilimia 78.3 ya lengo la 90 ya kwanza. Miongoni mwao wanaume walikuwa 413,985 sawa na asilimia 33, na wanawake walikuwa 838,220 sawa na asilimia 77″.alisema. Kwa upande wa vijana Waziri Ummy amesema kuwa Vijana balehe (umri wa miaka 10 â 19) walikuwa 57,167 sawa na asilimia 4.6, na vijana (umri wa miaka 15 â 24) walikuwa 96,006 sawa na asilimia 7.7. Aidha, amesema kati ya waliopima na kutambua afya zao watu 1,221,799 sawa na asilimia 97.6 wanatumia ARV. Hata hivyo alisema Lengo la 90 ya pili ambalo ni asilimia ya kuwa watu waliopimwa na kugundulika kuwa wana maambukizi ya VVU wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU (yaani ARVâs), tayari tumefikia takriban asilimia 98 wanatumia zawa za kupunguza makali ya VVU yaani ARV. “Lengo la 90 ya tatu, ambalo ni kuhakikisha kuwa asilimia 90 ya wanaotumia ARVâs wamefanikiwa kupunguza wingi wa VVU mwilini Waziri huyo alisema wamefanya vizuri sana,”ni kuwa tumekuwa tukifuatilia kwa karibu hali za watu wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU”.Alisema.
Maambukizi ya VVU yapungua kwa 2.3% kwa miaka 13
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003/4 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016/17 .
Ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa kujadili maendeleo ya utekelezaji wa sera ya pamoja ya ushirikiano na Serikali ya Marekani kupitia Pepfar cop 19 ya utekelezaji wa sera ya VVU na UKIMWI uliofanyika jijini Dar Es Salaam.
âKuanzia huduma za UKIMWI zianze kutolewa nchini tumeshuhudia mafanikio makubwa kwa upande wa kupunguza maambukizi kutoka asilimia 7 mwaka 2003/4 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016/17″ alisema Waziri Ummy.
Aliendelea kusema kuwa Serikali imefanikiwa kutoa huduma za utambuzi na matibabu na sasa dhana ya kwamba UKIMWI ni ugonjwa wa kifo imeisha na kuwa ni ugonjwa unaoweza kudhibitiwa
Aidha,Waziri Ummy amesema kuwa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo PEPFAR inaendelea kupanga mikakati mbalimbali ya kudhibiti maambukizi ya UKIMWI, kutoa huduma na matibabu kwa watu wanaoishi na virusi.
Mbali na hayo Waziri Ummy amedai kuwa Serikali imefanikiwa kutoa huduma za utambuzi na matibabu, huku akisisitiza kuwa dhana ya kwamba UKIMWI ni ugonjwa wa kifo imeisha baina ya wananchi
Hata hivyo, Waziri Ummy amesema, kufikia mwezi Septemba mwaka 2019 idadi ya watu waliopima na kujua afya zao imefikia asilimia 77.2 na kati yao asilimia 98 wanaendelea na huduma za VVU pamoja na matumizi ya ARV.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Dr. Inmi Patterson amesema Serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ugonjwa wa UKIMWI na ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa jitihada kubwa inazofanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kudhibiti maambukizi na kutoa huduma bora za VVU kwa watu waliogundulika na maambukizi.
Mkutano huo ulijumuisha wadau mbalimbali akiwemo mwakilishi wa Shirika la Afya duniani nchini Tanzania Dkt. Tigest Ketsela pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa kinga Dkt. Leonard Subi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tume ya kudhibiti na kupambana na UKIMWI (TACAIDS) pamoja na Shirika la PEPFAR Tanzania.
Wanaume zaidi ya milioni nne nchini wafanyiwa tohara â Dodoma
JUMLA ya wanaume milioni 4,456,511 wamefanyiwa tohara kinga ya kitabibu tangu 2009 ilipoanza kutolewa hadi kufikia Septemba, 2019.
Hayo yamesemwa na Afisa Mpango kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Sasan Mmbando wakati wa semina ya kuwajengea uelewa wabunge wa Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Kamati yabkudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na kamati ya Katiba na Sheria kuhusu mpango huo. Dk. Mmbando alisema kuwa lengo la kwanza la afua hiyo lilikuwa kuwafikia wanaume na vijana milioni 2.8 kufikia Septemba, 2017.âHadi kufikia Septemba, 2017 tumeweza kuwafikia milioni 3,303,940 na kuwatahiri,â alisema.
Aidha, alisema katika lengo la pili kuanzia mwaka 2017 hadi 2022 wana mpango wa kuwafikia wanaume milioni 2.7. Alisema hadi kufikia Septemba, 2019, tayari wameweza kuwatahiri jumla ya wanaume 1,681,070 ikiwa ni sawa na asilimia 60 ya lengo. Alisema afua hiyo inatekelezwa katika mikoa 17 yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya HIV na kiwango kidogo cha utahiri nchini.
âHata hivyo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ili kuwa na huduma endelevu na kupunguza matatizo ya njia ya mkojo, mfano UTI, ilianza kutoa huduma ya tohara kwa watoto wachanga wenye umri kuanzia siku moja hadi 60, 2013, kama utafiti wa kujifunzia (pilot study), katika mkoa wa Iringa hadi sasa imefikia mikoa 15 nchini,â alibainisha. Alisema hadi kufikia Septemba, 2019 jumla ya watoto wachanga 13,603 wametahiriwa.âTohara ya watoto wachanga inafanyika katika mikoa 15, Iringa Njombe, Morogoro, Singida, Tabora, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera, Rukwa, Katavi, Songwe, Mbeya na Kigoma,â alisema.
Waziri aongea na waandishi kuhusu mkutano wa mawaziri wa sekta ya afya na UKIMWI wa nchi za SADC
Baada ya kupokea uenyekiti wa SADC mwezi Agosti 2019, Tanzania itakuwa mwenyeji wa mikutano ya kisekta ukiwemo mkutano wa Mawaziri wa sekta ya Afya na UKIMWI utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 4-8 Novemba 2019.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni âUshirikiano wa Nchi za SADC ni Nguzo Kuu kufikia Maendeleo Endelevu ya Sekta ya Afya na Mapambano dhidi ya UKIMWI. Mkutano utafunguliwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mkutano wa Mawaziri unalenga kuangalia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC ya mwaka 1999 na mpango Mkakati wa Kanda kuhusu masuala ya afya pamoja na kuridhia kwa pamoja maazimio mbalimbali kuhusu masuala ya afya yatakayojadili2a kwenye mkutano huo.
Agenda muhimu zitakazojadiliwa zitahusu magonjwa yanayoziathiri nchi za SADC ikiwemo UKIMWI, Kifua Kikuu (TB), Malaria na masuala ya Lishe, afya uzazi, mama na mtoto na ugonjwa wa Ebola. UKIMWI bado ni changamoto katika nchi za SADC. Tanzania imepunguza maambukizi kutoka asilimia 7 mwaka 2003 hadi asilimia 4.7 mwaka 2017
Nchi za SADC zimejielekeza kutekeleza malengo ya
kimataifa ya Kutokomeza UKIMWI kwa kutumia mkakati ujulikanao kama
909090(tisini tatu) yaani
*Tisini ya kwanza Kuhamasisha watu kupima na kutambua hali zao kiafya
*Tisini ya pili wenye maambukizi wawe wanatumia dawa
*Tisini ya tatu Kuhakikisha wanaotumia ARVs wawe wamefubaza
Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye mzigo mkubwa wa ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na ni miongoni mwa nchi tano za SADC zinazokabiliwa na tatizo hilo. Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 duniani zilizopiga hatua kubwa katika kuwaibua wahisiwa wa ugonjwa wa kifua kikuu.
Matibabu ya Kifua kikuu yapo na watu wakitumia dawa ipasavyo wanapona. Kutokomeza ugonjwa wa Kifua kikuu ni kipaumbele cha nchi za SADC.Tanzania itatuma fursa ya mkutano huo kukitangaza kiwanda cha viuadudu wa malaria cha Labiofam kilichopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani ili kupata soko la dawa zinazozalishwa kiwandani hapo
Tanzania itatumia fursa ya ziara ya Mawaziri kiwandani hapo tarehe 8 Novemba 2019 kuzindua kampeni ya kitaifa dhidi ya ugonjwa wa malaria ijulikanayo kama “Zero Malaria starts with me”(Zero Malaria inaanza na mimi) itakayofanyika tarehe 8 Novemba 2019.
Kasi ya maambukizi ya malaria imepungua kutoka asilimia 16.7 mwaka 2015 hadi asilimia 7 mwaka 2017. Changamoto ya utapiamlo na uzito uliopitiliza kwa nchi za SADC itajadiliwa kwenye mkutano huo
Tanzania itatumia mkutano huo kutangaza shughuli za Bohari ya Dawa (MSD) ambayo ilishinda zabuni ya kufanya Ununuzi wa pamoja wa dawa, vifaa na vifaa tiba kwa nchi za SADC. Mkutano utajadili afya ya uzazi,mama na mtoto kwa kuangalia namna ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito, chanjo kwa watoto na kuimarisha afya kwa wasichana balehe. Mawaziri watajadili huduma za kukabiliana na majanga na dharura ikiwemo namna ya kushirikiana katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola.
Sheria za Kimataifa kuhusu masuala ya afya kwa wote yatajadiliwa.Nikiwa Mwenyekiti wa Mkutano huo, nitasimamia hoja za Tanzania ikiwemo kuzishauri nchi wanachama kuwekeza kwenye afya bora ambayo ni msingi wa maendeleo na ukuaji wa uchumi; kuendelea kukabiliana na magonjwa yanayozuilika na nchi wanachama kuwa na huduma zenye Sawa kwa wote. Tanzania anaamini kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba.