Waziri Gwajima Akutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt. Gorothy Gwajima ameongoza timu ya Wataalamu wa wa Wizara yake katika kikao na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya chini ya Makamu Mwenyekiti Mh. Dkt. Alice Karungi Kaijage.
Semina elekezi ya VVU na UKIMWI imewaleta wasanii wa aina mbalimbali ili waweze kuelewa zaidi kuhusu utaratibu wa sasa wa upimaji VVU na utumiaji wa ARV.
Makamu wa Rais Afungua Mkutano wa Afya na Ukimwi wa Mawaziri SADC
Makamu wa Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan Akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam, kufungua Mkutano wa Mawaziri wa Afya na UKIMWI Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) leo Novemba 07, 2019
Wanaume milioni 4,456,511 wamefanyiwa tohara kinga ya kitabibu tangu 2009 ilipoanza kutolewa hadi kufikia Septemba, 2019.
Hayo yamesemwa na Afisa Mpango kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk. Susan Mmbando wakati wa semina ya kuwajengea uelewa wabunge wa Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Kamati yabkudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na kamati ya Katiba na Sheria kuhusu mpango huo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003/4 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016/17
Waziri Wa Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia Wazee Na Watoto Mh.Ummy Mwalimu Wakati Akiongea Na Waandishi Wa Habari Kuhusu Mkutano Wa Mawaziri Wa Sekta Afya Na Ukimwi Wa Nchi Za Sadc Leo Tarehe 29 Oktoba 2019