Baada ya kupokea uenyekiti wa SADC mwezi Agosti 2019, Tanzania itakuwa mwenyeji wa mikutano ya kisekta ukiwemo mkutano wa Mawaziri wa sekta ya Afya na UKIMWI utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 4-8 Novemba 2019.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni âUshirikiano wa Nchi za SADC ni Nguzo Kuu kufikia Maendeleo Endelevu ya Sekta ya Afya na Mapambano dhidi ya UKIMWI. Mkutano utafunguliwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mkutano wa Mawaziri unalenga kuangalia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC ya mwaka 1999 na mpango Mkakati wa Kanda kuhusu masuala ya afya pamoja na kuridhia kwa pamoja maazimio mbalimbali kuhusu masuala ya afya yatakayojadili2a kwenye mkutano huo.
Agenda muhimu zitakazojadiliwa zitahusu magonjwa yanayoziathiri nchi za SADC ikiwemo UKIMWI, Kifua Kikuu (TB), Malaria na masuala ya Lishe, afya uzazi, mama na mtoto na ugonjwa wa Ebola. UKIMWI bado ni changamoto katika nchi za SADC. Tanzania imepunguza maambukizi kutoka asilimia 7 mwaka 2003 hadi asilimia 4.7 mwaka 2017
Nchi za SADC zimejielekeza kutekeleza malengo ya
kimataifa ya Kutokomeza UKIMWI kwa kutumia mkakati ujulikanao kama
909090(tisini tatu) yaani
*Tisini ya kwanza Kuhamasisha watu kupima na kutambua hali zao kiafya
*Tisini ya pili wenye maambukizi wawe wanatumia dawa
*Tisini ya tatu Kuhakikisha wanaotumia ARVs wawe wamefubaza
Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye mzigo mkubwa wa ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na ni miongoni mwa nchi tano za SADC zinazokabiliwa na tatizo hilo. Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 duniani zilizopiga hatua kubwa katika kuwaibua wahisiwa wa ugonjwa wa kifua kikuu.
Matibabu ya Kifua kikuu yapo na watu wakitumia dawa ipasavyo wanapona. Kutokomeza ugonjwa wa Kifua kikuu ni kipaumbele cha nchi za SADC.Tanzania itatuma fursa ya mkutano huo kukitangaza kiwanda cha viuadudu wa malaria cha Labiofam kilichopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani ili kupata soko la dawa zinazozalishwa kiwandani hapo
Tanzania itatumia fursa ya ziara ya Mawaziri kiwandani hapo tarehe 8 Novemba 2019 kuzindua kampeni ya kitaifa dhidi ya ugonjwa wa malaria ijulikanayo kama “Zero Malaria starts with me”(Zero Malaria inaanza na mimi) itakayofanyika tarehe 8 Novemba 2019.
Kasi ya maambukizi ya malaria imepungua kutoka asilimia 16.7 mwaka 2015 hadi asilimia 7 mwaka 2017. Changamoto ya utapiamlo na uzito uliopitiliza kwa nchi za SADC itajadiliwa kwenye mkutano huo
Tanzania itatumia mkutano huo kutangaza shughuli za Bohari ya Dawa (MSD) ambayo ilishinda zabuni ya kufanya Ununuzi wa pamoja wa dawa, vifaa na vifaa tiba kwa nchi za SADC. Mkutano utajadili afya ya uzazi,mama na mtoto kwa kuangalia namna ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito, chanjo kwa watoto na kuimarisha afya kwa wasichana balehe. Mawaziri watajadili huduma za kukabiliana na majanga na dharura ikiwemo namna ya kushirikiana katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola.
Sheria za Kimataifa kuhusu masuala ya afya kwa wote yatajadiliwa.Nikiwa Mwenyekiti wa Mkutano huo, nitasimamia hoja za Tanzania ikiwemo kuzishauri nchi wanachama kuwekeza kwenye afya bora ambayo ni msingi wa maendeleo na ukuaji wa uchumi; kuendelea kukabiliana na magonjwa yanayozuilika na nchi wanachama kuwa na huduma zenye Sawa kwa wote. Tanzania anaamini kuwa “Kinga ni bora kuliko tiba.